Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 45

45
Koreshi, chombo cha Mungu
1 # Zab 73:23; Isa 41:13 Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi#45:1 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme;#45:1 Katika Kiebrania ni: Nitalegeza viuno vya wafalme. ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. 2Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma; 3#Kut 33:12 nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. 4#Isa 44:1; Mdo 17:23; Gal 1:8,9; Efe 2:12; 1 The 4:5 Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. 5#Kum 4:35; Zab 18:32 Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha#45:5 Katika Kiebrania ni: kufunga mshipi. ijapokuwa hukunijua; 6#Zab 102:15; Mal 1:11 ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine. 7#Amo 3:6 Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
8 # Zab 85:11 Dondokeni, enyi mbingu, toka juu,
Mawingu na yamwage haki;
Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu,
Nayo itoe haki ikamee pamoja;
Mimi, BWANA, nimeiumba.
9 # Rum 9:20; Isa 64:8; Yer 18:6 Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unatengeneza nini? Au chombo ulichotengeneza hakina mikono? 10Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una uchungu wa kujifungua nini? 11#Yer 31:9; Isa 29:23 BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni. 12#Yer 27:5 Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru. 13#Ezr 1:1; Rum 3:24 Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.
14 # Zab 68:31; Isa 49:23; Zek 8:22; 1 Kor 14:25 BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena. 15#Kum 29:29; Zab 36:6; Isa 8:17; Rum 11:33 Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi. 16Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale watengenezao sanamu wataingia fadhaa pamoja. 17#2 Sam 23:5; Zab 103:17; Hos 1:7; Rum 11:26 Bali Israeli wataokolewa na BWANA kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.
18Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine. 19#Kum 30:11; Neh 9:13; Zab 19:8; Rum 7:12 Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, BWANA, nasema ukweli; nanena mambo ya haki.
Miungu haiwezi kuokoa Babeli
20 # Yer 44:28; Rum 1:22 Jikusanyeni mje; na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa mliookoka; hawana maarifa wale wachukuao mti wa sanamu yao ya kuchonga; wamwombao mungu asiyeweza kuokoa. 21Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi. 22Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. 23#Mwa 22:16; Yer 22:5; Ebr 6:13; Mwa 31:53; Kum 6:13; Zab 63:11; Rum 14:11; Flp 2:10-11 Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa. 24Mmoja ataniambia, Kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika. 25Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 45: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia