Isaya 40:1-2
Isaya 40:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu wenu asema: “Wafarijini watu wangu, nendeni mkawafariji. Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole, waambieni kwamba utumwa wao umekwisha, wamesamehewa uovu wao. Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufu kwa sababu ya dhambi zao zote.”
Isaya 40:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Isaya 40:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Isaya 40:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wafarijini, wafarijini watu wangu, asema Mungu wenu. Sema na Yerusalemu kwa upole, umtangazie kwamba kazi yake ngumu imekamilika, kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia, kwamba amepokea kutoka mkononi mwa BWANA maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote.