Isaya 21:11-17
Isaya 21:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Kauli ya Mungu dhidi ya Duma. Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri: “Mlinzi, nini kipya leo usiku? Kuna kipya chochote leo usiku?” Nami mlinzi nikajibu: “Asubuhi inakuja, kadhalika na usiku; ukitaka kuuliza, uliza tu; nenda urudi tena.” Kauli ya Mungu dhidi ya Arabia. Enyi misafara ya Dedani, pigeni kambi leo usiku kwenye nyika za Arabia. Enyi wakazi wa nchi ya Tema, wapeni maji hao wenye kiu; wapelekeeni chakula hao wakimbizi. Maana wamekimbia mapanga, mapanga yaliyochomolewa, pinde zilizovutwa na ukali wa mapigano. Maana Bwana aliniambia hivi: “Katika muda wa mwaka mmoja, bila kuzidi wala kupungua, fahari yote ya Kedari itakwisha. Wapiga upinde wachache kati ya mashujaa wa watu wa Kedari ndio watakaosalia. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Isaya 21:11-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena. Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani. Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao. Kwa maana wanakimbia mbele ya panga, Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa, Na mbele ya ukali wa vita. Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari. Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.
Isaya 21:11-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Isaya 21:11-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Neno kuhusu Duma: Mtu fulani ananiita kutoka Seiri, “Mlinzi, usiku utaisha lini? Mlinzi, usiku utaisha lini?” Mlinzi anajibu, “Asubuhi inakuja, lakini pia usiku. Kama ungeliuliza, basi uliza; bado na urudi tena.” Neno kuhusu Arabia: Enyi misafara ya Wadedani, mnaopiga kambi katika vichaka vya Arabia, leteni maji kwa wenye kiu, ninyi mnaoishi Tema, leteni chakula kwa ajili ya wakimbizi. Wanaukimbia upanga, kutoka upanga uliochomolewa alani, kutoka upinde uliopindwa, na kutoka kwenye joto la vita. Hili ndilo Bwana analoniambia: “Katika muda wa mwaka mmoja, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, majivuno yote ya Kedari yatafikia mwisho. Wanaume wavutao pinde walionusurika, mashujaa wa Kedari, watakuwa wachache.” BWANA, Mungu wa Israeli, amesema.