Isaya 19:18-25
Isaya 19:18-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu. Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, na nguzo mpakani mwake kwa BWANA. Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa. Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza. Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya. Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri. Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia; kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
Isaya 19:18-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku hiyo lugha ya Kiebrania itatumika katika miji mitano ya Misri, na watu wa miji hiyo wataapa kuwa waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mji mmojawapo utaitwa “Mji wa Jua.” Siku hiyo, kutakuwa na madhabahu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu katikati ya nchi ya Misri, na nguzo iliyowekwa wakfu kwa Mungu kwenye mpaka wa Misri. Madhabahu hiyo itakuwa ishara na ushuhuda kwake Mwenyezi-Mungu wa majeshi katika nchi ya Misri. Watu wakimlilia Mwenyezi-Mungu humo kwa sababu ya kukandamizwa, yeye atawapelekea mkombozi atakayewatetea na kuwakomboa. Mwenyezi-Mungu atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomkiri na kumwabudu kwa kumtolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Hali kadhalika, watamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri ambazo watazitimiza. Mwenyezi-Mungu atawaadhibu Wamisri na kuwaponya. Nao watamrudia, naye atayasikiliza maombi yao na kuwaponya. Wakati huo, kutakuwa na barabara kuu kutoka nchi ya Misri hadi nchi ya Ashuru. Waashuru watawatembelea Wamisri, na Wamisri watawatembelea Waashuru; nao wote watamwabudu Mungu pamoja. Wakati huo, Israeli itahesabiwa pamoja na Misri na Ashuru; mataifa haya matatu yatakuwa baraka kwa dunia yote. Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawabariki na kusema, “Wabarikiwe Wamisri watu wangu, kadhalika na Waashuru ambao ni ishara ya kazi yangu na Waisraeli walio mali yangu.”
Isaya 19:18-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa jua. Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, na nguzo mpakani mwake kwa BWANA. Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi wa kuwatetea, naye atawaokoa. Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza. Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya. Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hadi Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri. Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka katika dunia; kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
Isaya 19:18-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu. Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, na nguzo mpakani mwake kwa BWANA. Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa. Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza. Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya. Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri. Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia; kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
Isaya 19:18-25 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Mji mmoja utaitwa Mji wa Uharibifu. Katika siku hiyo patakuwa na madhabahu ya Mwenyezi Mungu katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa Mwenyezi Mungu kwenye mpaka wa Misri. Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. Hivyo Mwenyezi Mungu atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Mwenyezi Mungu. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Mwenyezi Mungu nadhiri na kuzitimiza. Mwenyezi Mungu ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Mwenyezi Mungu, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya. Katika siku hiyo kutakuwa na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru wataenda Misri, na Wamisri wataenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja. Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia. Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.”