Habakuki 3:7-13
Habakuki 3:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Niliwaona watu wa Kushani wakiteseka, na watu wa Midiani wakitetemeka. Ee Mwenyezi-Mungu, je, umeikasirikia mito? Je, umeyakasirikia maji ya bahari, hata ukaendesha farasi wako, na magari ya vita kupata ushindi? Uliuweka tayari uta wako, ukaweka mishale yako kwenye kamba. Uliipasua ardhi kwa mito. Milima ilikuona, ikanyauka; mafuriko ya maji yakapita humo. Vilindi vya bahari vilinguruma, na kurusha juu mawimbi yake. Jua na mwezi vilikaa kimya katika makazi yao, vilipoona miali ya mishale yako ikienda kasi, naam, vilipouona mkuki wako ukimetameta. Kwa ghadhabu ulipita juu ya nchi, uliyakanyaga mataifa kwa hasira yako. Ulitoka kwenda kuwaokoa watu wako, kumwokoa yule uliyemweka wakfu kwa mafuta. Ulimponda kiongozi wa jamii ya waovu, ukawaangamiza kabisa wafuasi wake.
Habakuki 3:7-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Niliziona hema za Kushani zikitaabika; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka. Je! BWANA aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi wako, Katika magari yako ya wokovu? Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito. Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake. Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao. Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
Habakuki 3:7-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naliziona hema za Kushani katika taabu; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka. Je! BWANA aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi zako, Katika magari yako ya wokovu? Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito. Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake. Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao. Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
Habakuki 3:7-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Niliona watu wa Kushani katika dhiki, na makazi ya Midiani katika maumivu makali. Ee BWANA, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi? Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito; milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu. Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao. Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa. Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.