Mwanzo 37:5-7
Mwanzo 37:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Mwanzo 37:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”
Mwanzo 37:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiku mmoja, Yosefu aliota ndoto, lakini alipowasimulia ndugu zake, wao wakazidi kumchukia. Aliwaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: Niliota kuwa sote tulikuwa shambani tukifunga miganda na ghafla mganda wangu ukainuka na kusimama wima. Miganda yenu ikakusanyika kuuzunguka na kuuinamia mganda wangu.”
Mwanzo 37:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)