Mwanzo 11:6-7
Mwanzo 11:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa. Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Mwanzo 11:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
Mwanzo 11:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)