Mwanzo 11:24-32
Mwanzo 11:24-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. Hawa ndio wazao wa Tera. Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.
Mwanzo 11:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Nahori alipokuwa na umri wa miaka 29, alimzaa Tera. Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka 119, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Wafuatao ni wazawa wa Tera, baba yao Abramu, Nahori na Harani. Harani alikuwa baba yake Loti. Huyo Harani alifariki wakati Tera baba yake alikuwa anaishi huko Uri alikokuwa amezaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai. Mke wa Nahori aliitwa Milka, binti Harani ambaye pia alikuwa baba yake Iska. Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa. Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205.
Mwanzo 11:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nahori akaishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.
Mwanzo 11:24-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.