Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 11:24-32

Mwanzo 11:24-32 NENO

Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka mia moja na kumi na tisa (119), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na baadaye akawazaa Nahori na Harani. Hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Lutu. Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa katika Uru ya Wakaldayo, nchi aliyozaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, naye mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. Tera akawachukua Abramu mwanawe, mjukuu wake Lutu mwana wa Harani, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka Uru ya Wakaldayo pamoja, wakaenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. Tera aliishi miaka mia mbili na mitano (205), akafa huko Harani.