Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 6:1-14

Ezekieli 6:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu, igeukie milima ya Israeli, utangaze ujumbe huu wangu dhidi ya wakazi wake na kusema: Sikilizeni neno la Bwana Mwenyezi-Mungu enyi wakazi wa milima ya Israeli: Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambieni nyinyi wakazi wa milimani na vilimani, wa magengeni na mabondeni kwamba mimi mwenyewe nitaleta upanga na kuharibu sehemu zenu zote zilizoinuka za ibada. Madhabahu zenu zitaharibiwa na mahali penu pa kufukizia ubani patavunjwavunjwa. Wale watakaouawa nitawatupa mbele ya sanamu zenu za miungu. Maiti za Waisraeli nitazilaza mbele ya sanamu zao za miungu, na mifupa yenu nitaitawanya kandokando ya madhabahu zenu. Kokote mnakoishi, miji yenu itakuwa ukiwa na sehemu za mwinuko za ibada zenu zitabomolewa, madhabahu zenu ziwe uharibifu na maangamizi, sanamu zenu za miungu zivunjwe na kuharibiwa. Mahali penu pa kufukizia ubani patabomolewa na chochote mlichofanya kitatokomezwa. Wale watakaouawa wataanguka kati yenu, nanyi mtatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu. “Hata hivyo, nitawaacha wengine wabaki hai; baadhi yenu watanusurika kuuawa nao watatawanyika katika nchi mbalimbali. Ndipo watakaponikumbuka mimi miongoni mwa hao watu wa mataifa ambamo watatawanyika. Watakumbuka jinsi nilivyowapiga kwa sababu mioyo yao isiyo na uaminifu ilinigeuka na kwa vile waliacha kunitazamia mimi wakazitazamia sanamu za miungu. Kwa hiyo watajichukia wao wenyewe kwa sababu ya maovu na machukizo yao yote waliyoyatenda. Hapo ndipo watakapojifunza kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu; sikuwatisha bure ya kwamba nitawaletea maovu hayo yote.” Bwana Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Piga makofi, piga kishindo kwa mguu na kusema: Ole wenu Waisraeli kwa sababu ya machukizo yenu yote, kwani mtakufa kwa upanga, njaa na kwa maradhi mabaya. Aliye mbali sana atakufa kwa maradhi mabaya. Aliye karibu atauawa kwa upanga. Atakayekuwa amebaki na kunusurika hayo mawili atakufa kwa njaa. Ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao. Maiti zao zitatapakaa kati ya sanamu zao za miungu na madhabahu zao, juu ya kila mlima, chini ya kila mti mbichi, chini ya kila mwaloni wenye majani na kila mahali walipotolea tambiko zao za harufu nzuri ya kuzipendeza sanamu zao za miungu. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Nitaunyosha mkono wangu dhidi yao, na kuiharibu nchi yao. Tangu huko jangwani kusini mpaka mjini Ribla kaskazini, nitaifanya nchi yao kuwa mahame kabisa wasipate mahali pa kuishi. Hapo ndipo wote watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Shirikisha
Soma Ezekieli 6

Ezekieli 6:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame milima ya Israeli, ukaitabirie, ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, Na madhabahu zenu zitakuwa ukiwa, na sanamu zenu za jua zitavunjika; nami nitawatupa wana wenu waliouawa mbele ya vinyago vyenu. Nami nitaiweka mizoga ya wana wa Israeli mbele ya vinyago vyao; nami nitaitawanya mifupa yenu pande zote za madhabahu zenu. Kila mahali mkaapo miji itaharibika, na mahali palipoinuka patakuwa ukiwa; ili madhabahu zenu ziharibiwe, na kufanywa ukiwa, na vinyago vyenu vivunjwe, na kukoma, na sanamu zenu za jua zikatwe, na kuangushwa, na kazi zenu zifutwe kabisa. Na hao waliouawa wataanguka katikati yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Lakini nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu. Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa, watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba, iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote, waliyoyatenda kwa machukizo yao yote. Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; sikusema bure kama nitawatenda mabaya hayo. Bwana MUNGU asema hivi; Piga kwa mkono wako, ipige nchi kwa mguu wako, ukaseme, Ole! Kwa sababu ya machukizo maovu yote ya nyumba ya Israeli; maana wataanguka kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni. Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni; na yeye aliye karibu atakufa kwa upanga; na yeye atakayesalia, na kuhusuriwa katika mji, atakufa kwa njaa, hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu juu yao. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, watu wa kwao waliouawa watakapokuwa kati ya vinyago vyao, pande zote za madhabahu zao, juu ya kila kilima kirefu, juu ya vilele vya milima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, na chini ya kila mwaloni mnene, pale pale walipovifukizia uvumba mzuri vinyago vyao vyote. Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Shirikisha
Soma Ezekieli 6

Ezekieli 6:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ezekieli 6:1-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Neno la BWANA likanijia kusema, “Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la BWANA Mwenyezi. Hili ndilo BWANA Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu. Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu. Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu. Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali. Watu wenu watachinjwa katikati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi BWANA. “ ‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa watakapokuwa wametawanyika katika nchi na mataifa. Ndipo katika mataifa ambamo watakuwa wamechukuliwa mateka, wale ambao watanusurika watanikumbuka, jinsi ambavyo nimehuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi, ambayo imegeukia mbali nami na macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa ajili ya uovu walioutenda na kwa ajili ya desturi zao za kuchukiza. Nao watajua kuwa Mimi ndimi BWANA, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao. “ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni. Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao. Nao watajua kwamba Mimi ndimi BWANA, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala katikati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani, sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote. Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi BWANA.’ ”

Shirikisha
Soma Ezekieli 6