Ezekieli 48:1-7
Ezekieli 48:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi. “Asheri atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi. “Naftali atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi. “Manase atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi. “Efraimu atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi. “Reubeni atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi. “Yuda atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.
Ezekieli 48:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani. Eneo linalopakana na la Dani, kutoka mashariki hadi magharibi litakuwa la Asheri. Kabila la Naftali, litapata eneo linalopakana na lile la Asheri, kutoka mashariki hadi magharibi. Baada ya eneo la kabila la Naftali, litafuata eneo la kabila la Manase, kutoka mashariki hadi magharibi. Eneo linalopakana na eneo la Manase, kutoka upande wa mashariki hadi magharibi, litakuwa la kabila la Efraimu. Eneo linalopakana na eneo la Efraimu, kutoka mashariki hadi magharibi, litakuwa la kabila la Reubeni. Eneo linalopakana na eneo la Reubeni, kutoka mashariki hadi magharibi litakuwa la kabila la Yuda.
Ezekieli 48:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja. Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Asheri, fungu moja. Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja. Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Manase, fungu moja. Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja. Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja. Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
Ezekieli 48:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, haya ndiyo majina ya kabila hizo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hata maingilio ya Hamathi, hata Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja. Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Asheri, fungu moja. Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Naftali, fungu moja. Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Manase, fungu moja. Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja. Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja. Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.