Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 48:1-7

Ezekieli 48:1-7 NENO

“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja; mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi; Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi. Asheri atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi. Naftali atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi. Manase atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi. Efraimu atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi. Reubeni atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi. Yuda atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.