Ezekieli 25:1-17
Ezekieli 25:1-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu! Wageukie Waamoni, ukatoe unabii dhidi yao. Waambie Waamoni: Sikilizeni neno la Bwana Mwenyezi-Mungu: Nyinyi mlifurahia kuona maskani yangu ikitiwa unajisi, nchi ya Israeli ikiangamizwa na watu wa Yuda wakipelekwa uhamishoni. Basi, nitawatia nyinyi mikononi mwa watu wa mashariki; watapiga hema zao kati yenu na kufanya makazi yao katika nchi yenu. Nao watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu. Mji wa Raba nitaufanya kuwa malisho ya ngamia na nchi ya Amoni zizi la kondoo. Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa sababu mlipiga makofi, mkarukaruka kwa furaha na kushangilia sana juu ya nchi ya Israeli, basi, mimi nimeunyosha mkono dhidi yenu; nitawaacha mtekwe nyara na watu wa mataifa mengine. Nitawaangamizeni, nanyi hamtakuwa taifa tena wala kuwa na nchi. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Bwana Mwenyezi-Mungu alisema: “Kwa kuwa Moabu imesema kuwa Yuda ni sawa tu na mataifa mengine, mimi nitaifanya miji inayolinda mipaka ya Moabu ishambuliwe, hata miji ile bora kabisa, yaani Beth-yeshimothi, Baal-meoni na Kiriathaimu. Nitaitia nchi hiyo pamoja na nchi ya Amoni mikononi mwa watu wa mashariki iwe mali yao. Nchi ya Moabu haitakuwa taifa tena. Mimi nitaiadhibu nchi ya Moabu, nao watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Bwana Mwenyezi-Mungu alisema hivi: “Kwa kuwa Waedomu wamefanya kisasi na Yuda, wakawalipiza watu wa Yuda kisasi kibaya sana basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Nitanyosha mkono dhidi ya nchi ya Edomu na kuwaua watu wote na wanyama. Nitaifanya kuwa ukiwa kutoka mji wa Temani hadi mji wa Dedani, watu watauawa kwa upanga. Nitawafanya watu wangu Israeli walipize kisasi juu ya Waedomu nao watawatenda Waedomu kadiri ya hasira na ghadhabu yangu. Ndipo Waedomu watakapotambua uzito wa kisasi changu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nimesema.” Bwana Mwenyezi-Mungu alisema hivi: “Kwa kuwa Wafilisti walifanya kisasi, wakawalipiza kisasi adui zao kwa ubaya sana na kuendelea kuwa maadui zao daima, basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitanyosha mkono dhidi ya Wafilisti; nitawaangamiza hao Wakerethi na wakazi wa pwani. Nitawalipiza kisasi kikali kwa adhabu ya ghadhabu. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Ezekieli 25:1-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, uwaelekezee wana wa Amoni uso wako, ukatabiri juu yao. Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni; basi, kwa sababu hiyo, nitakutia katika mikono ya wana wa mashariki uwe milki yao, nao watajenga kambi yao ndani yako, kufanya maskani zao ndani yako; watakula matunda yako, na kunywa maziwa yako. Nami nitafanya Raba kuwa banda la ngamia, na wana wa Amoni kuwa mahali pa kulaza makundi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako; basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na makabila ya watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote; basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu, pamoja na wana wa Amoni, nami nitawatoa kuwa milki, ili wana wa Amoni wasikumbukwe kati ya mataifa, nami nitatoa hukumu juu ya Moabu; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao; kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga. Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima; kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani. Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapojilipiza kisasi juu yao.
Ezekieli 25:1-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, uwaelekezee wana wa Amoni uso wako, ukatabiri juu yao. Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni; basi, kwa sababu hiyo, nitakutia katika mikono ya wana wa mashariki uwe milki yao, nao wataweka marago yao ndani yako, kufanya maskani zao ndani yako; watakula matunda yako, na kunywa maziwa yako. Nami nitafanya Raba kuwa banda la ngamia, na wana wa Amoni kuwa mahali pa kulaza makundi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako; basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na kabila za watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote; basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu, pamoja na wana wa Amoni, nami nitawatoa kuwa milki, ili wana wa Amoni wasikumbukwe kati ya mataifa, nami nitatoa hukumu juu ya Moabu; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao; Oba 1-14; Mal 1:2-5 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga. Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa jeuri ya roho, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani. Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapojilipiza kisasi juu yao.
Ezekieli 25:1-17 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao. Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipoenda uhamishoni, kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao kati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu. Nitaufanya mji wa Raba kuwa malisho ya ngamia na Amoni kuwa mahali pa kondoo pa kupumzikia. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa mmepiga makofi yenu na kufanya kishindo kwa miguu, mkifurahia kwa mioyo yenu miovu juu ya yale mabaya yaliyoipata nchi ya Israeli, hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yenu na kuwatoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitawakatilia mbali kutoka mataifa na kuwang’oa kutoka nchi. Nitawaangamiza, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Moabu na Seiri wamesema, “Tazama, nyumba ya Yuda imekuwa kama mataifa mengine yote,” kwa hiyo nitaiondoa ile miji iliyo kando ya Moabu, kuanzia miji iliyo mipakani: Beth-Yeshimothi, Baal-Meoni na Kiriathaimu, iliyo utukufu wa nchi hiyo. Nitaitia Moabu pamoja na Waamoni mikononi mwa watu wa Mashariki kuwa milki yao, ili Waamoni wasikumbukwe miongoni mwa mataifa, nami nitatoa adhabu kwa Moabu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Edomu walilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda, wakakosea sana kwa kufanya hivyo, kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaunyoosha mkono wangu dhidi ya Edomu na kuua watu wake na wanyama wao. Nitaufanya ukiwa, na kuanzia Temani hadi Dedani wataanguka kwa upanga. Nitalipiza Edomu kisasi kwa mkono wa watu wangu Israeli, nao watawatendea Edomu sawasawa na hasira yangu na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Wafilisti wamewalipiza kisasi kwa uovu wa mioyo yao na kwa uadui wa siku nyingi wakataka kuangamiza Yuda, kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ninakaribia kuunyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi na kuwaangamiza wale waliosalia katika pwani. Nitalipiza kisasi kikubwa juu yao na kuwaadhibu katika ghadhabu yangu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapolipiza kisasi juu yao.’ ”