Kutoka 40:33-34
Kutoka 40:33-34 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi. Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Kutoka 40:33-34 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo, Mose akaikamilisha kazi yote. Kisha, lile wingu likalifunika lile hema la mkutano, na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukalijaza hema.
Kutoka 40:33-34 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi. Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Kutoka 40:33-34 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi. BWANA Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu.