Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 40:17-33

Kutoka 40:17-33 Biblia Habari Njema (BHN)

Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza mwaka wa pili baada ya kutoka Misri, hema la mkutano lilisimikwa. Mose aliweka vikalio vyake, akainua mbao zake, akashikamanisha pau zake na kusimamisha nguzo zake. Alitandaza pazia juu ya hema takatifu na kuweka kifuniko cha hema juu yake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Kisha alichukua vile vibao viwili vya mawe na kuviweka katika lile sanduku. Aliipitisha ile mipiko katika vikonyo vya sanduku na kukiweka kiti cha rehema juu yake. Kisha akaliweka lile sanduku la maamuzi ndani ya hema na kutundika pazia, na kwa namna hiyo akalisitiri sanduku la maamuzi, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aliweka meza ndani ya hema la mkutano, upande wa kaskazini, sehemu ya nje ya pazia, na juu yake akaipanga mikate iliyotolewa kwa Mwenyezi-Mungu, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alikiweka kinara ndani ya hema la mkutano, upande wa kusini, mkabala wa meza. Humo, mbele ya Mwenyezi-Mungu, akaziwasha taa zake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aliiweka ile madhabahu ya dhahabu katika hema, mbele ya pazia, na kufukiza ubani wenye harufu nzuri juu yake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alitundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu, akaweka hapo langoni mwa hema takatifu madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, akatolea juu yake sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Aliliweka birika la kutawadhia katikati ya hema la mkutano na madhabahu, na kutia maji ya kutawadha. Mose, Aroni na wanawe, wote walinawa mikono na miguu yao humo. Kila walipoingia ndani ya hema au walipokaribia ile madhabahu, walinawa, kama Mose alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo, Mose akaikamilisha kazi yote.

Shirikisha
Soma Kutoka 40

Kutoka 40:17-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa. Musa akaisimamisha maskani, akaviweka vitako vyake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake. Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku; kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia. Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini. Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia. Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akalitia pazia la mlango wa maskani. Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea. Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake; hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

Shirikisha
Soma Kutoka 40

Kutoka 40:17-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi ile maskani ilisimamishwa. Musa akaisimamisha maskani, akayaweka matako yake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake. Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku; kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia. Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini. Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia. Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akalitia pazia la mlango wa maskani. Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea. Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake; hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa. Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

Shirikisha
Soma Kutoka 40

Kutoka 40:17-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama BWANA alivyomwagiza. Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama BWANA alivyomwagiza. Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia na kupanga mikate juu yake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwagiza. Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu na kuziweka taa mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwagiza. Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama BWANA alivyomwagiza. Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu. Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama BWANA alivyomwagiza. Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama BWANA alivyomwagiza Mose. Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.

Shirikisha
Soma Kutoka 40