Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 35:20-29

Kutoka 35:20-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA. Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, akavileta. Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya BWANA; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yoyote ya huo utumishi, akauleta. Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawati, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri. Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi. Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani, na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri. Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.

Shirikisha
Soma Kutoka 35

Kutoka 35:20-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA. Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi, na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, akavileta. Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya BWANA; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yo yote ya huo utumishi, akauleta. Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri. Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi. Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani, na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri. Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.

Shirikisha
Soma Kutoka 35

Kutoka 35:20-29 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Mose, na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa BWANA, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA. Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta. Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa BWANA, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani. Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri. Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za BWANA kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya BWANA aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose.

Shirikisha
Soma Kutoka 35