Esta 2:19-20
Esta 2:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme. Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye.
Esta 2:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Wasichana walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa ameketi penye lango la mfalme. Esta alikuwa bado hajajitambulisha ukoo wala kabila lake kama Mordekai alivyokuwa amemwonya asifanye hivyo; naye Esta alimtii kama alivyokuwa akimtii wakati wa utoto wake, alipolelewa naye.
Esta 2:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme. Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye.
Esta 2:19-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati mabikira walikusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme. Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya kabila lake na uraia wake, kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.