Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta 2

2
Esta Afanywa malkia
1 # Est 1:19 Baada ya hayo, hasira yake mfalme Ahasuero ilipotulia, alimkumbuka Vashti, na vile alivyotenda, na yale yaliyoamriwa juu yake. 2#Mwa 12:14,15; 1 Fal 1:2 Basi watumishi wa mfalme waliomhudumia walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira vijana wazuri; 3naye mfalme aweke wasimamizi katika mikoa yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Susa, mji mkuu kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi wa nyumba ya mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso. 4Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza mfalme, naye akafanya hivyo.
5Basi palikuwa na Myahudi mmoja huko Susa, mji mkuu; jina lake Mordekai, mwana wa Yairi, mwana wa Shimei, mwana wa Kishi, wa kabila la Benyamini; 6#2 Fal 24:14,15; 2 Nya 36:10,20; Yer 22:24 ambaye alikuwa amechukuliwa mateka kutoka Yerusalemu miongoni mwa wafungwa waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda; ambaye Nebukadneza,#2:6 Au, Nebukadreza. mfalme wa Babeli, alimchukua. 7Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo nzuri na uso mwema; nao walipokufa baba yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake. 8Basi amri ya mfalme na mbiu yake iliposikiwa, wasichana wengi wakakusanyika huko Susa, mji mkuu mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake. 9Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na chakula chake, na vijakazi saba wa nyumbani mwa mfalme ili wamhudumie. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake. 10#Est 3:8; Law 26:36; Kum 28:65 Naye Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe. 11Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na yale yatakayompata.
12Basi zamu ya kila mwanamwali kuingia kwa mfalme Ahasuero, iliwadia baada ya kutayarishwa kulingana na sheria ya wanawake kwa miezi kumi na miwili; kwa kuwa ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake; 13mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila alichotaka alipewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme. 14Huenda jioni, na asubuhi hurudi katika nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa awe amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina. 15#Wim 6:9; Mdo 7:10; 2 Tim 4:18 Wakati ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona. 16#Est 3:7 Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kutawala kwake. 17#Mwa 41:40; 1 Sam 2:8; Est 3:14; Ayu 36:7; Zab 75:5; Lk 1:48,49; Yak 2:5; Ufu 3:21 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji la kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.
18 # Mwa 29:22; Amu 14:10; Est 1:3; Mt 25:1-10; Mk 6:21; Lk 14:8 Ndipo mfalme alipowafanyia karamu kubwa wakuu wake wote na watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya msamaha#2:18 Au msamaha wa kodi au siku ya mapumziko. katika majimbo yote, akatoa zawadi kulingana na ukarimu wa mfalme.
Mordekai Agundua Njama Langoni
19 # Est 3:2 Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi#2:19 Au alikuwa ameajiriwa kama msimamizi. mlangoni pa mfalme. 20Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye. 21Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili kati ya matowashi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, waliolinda milango ya vyumba vya mfalme, walikasirika sana, wakataka kumwua mfalme Ahasuero. 22#Est 6:1,2 Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai. 23#Mwa 40:19; Kum 21:22 Na jambo hilo lilipochunguzwa, na hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo pia yakaandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.

Iliyochaguliwa sasa

Esta 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha