Mhubiri 4:7-8
Mhubiri 4:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani. Nilimwona mtu mmoja asiye na mwana wala ndugu; hata hivyo, haachi kufanya kazi; hatosheki kamwe na mali yake; wala hatulii na kujiuliza: “Ninamfanyia nani kazi na kujinyima starehe?” Hilo nalo ni bure kabisa; ni shughuli inayosikitisha.
Mhubiri 4:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Mhubiri 4:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Mhubiri 4:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua: Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake, hakuwa na mwana wala ndugu. Hapakuwa na mwisho wa kazi yake, hata hivyo macho yake hayakutosheka na utajiri wake. Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani, nami kwa nini ninajinyima kufurahia?” Hili pia ni ubatili, ni shughuli yenye taabu!