Kumbukumbu la Sheria 5:32-33
Kumbukumbu la Sheria 5:32-33 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nyinyi muwe waangalifu mkafanye kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru; tekelezeni kila kitu barabara. Mtafuata njia yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata ili mambo yenu yawaendee vyema na mpate kuishi muda mrefu katika nchi mtakayotwaa iwe mali yenu.
Kumbukumbu la Sheria 5:32-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto. Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 5:32-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto. Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 5:32-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale BWANA Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. Fuateni yale yote ambayo BWANA Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.