Kumbukumbu la Sheria 32:44-47
Kumbukumbu la Sheria 32:44-47 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose alikuja mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, wakakariri maneno ya wimbo huu, ili Waisraeli wote wausikie. Mose alipomaliza kuwaambia watu wa Israeli maneno haya yote, aliwaambia, “Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo ninawapeni leo. Lazima muwaamuru watoto wenu ili wafuate kwa uaminifu maneno yote ya sheria hii. Maana sheria hii si maneno matupu bali ni uhai wenu; kwa sheria hii mtaishi maisha marefu katika nchi mnayokwenda kuimiliki, ngambo ya mto Yordani.”

Kumbukumbu la Sheria 32:44-47 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 32:44-47 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 32:44-47 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Musa na Yoshua mwana wa Nuni wakaja, wakanena maneno yote ya wimbo watu wakiwa wanasikia. Musa alipomaliza kuyasoma maneno haya yote kwa Israeli wote, akawaambia, “Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii. Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”