Kumbukumbu la Sheria 16:15
Kumbukumbu la Sheria 16:15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.
Kumbukumbu la Sheria 16:15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubariki katika mavuno yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Kumbukumbu la Sheria 16:15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Kumbukumbu la Sheria 16:15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya BWANA Mungu wenu katika mahali atakapopachagua BWANA. Kwa kuwa BWANA Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.