Amosi 3:9-15
Amosi 3:9-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake. Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao. Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara. Haya ndiyo asemayo BWANA; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya kochi, na juu ya mito ya hariri ya kitanda. Sikieni, mkashuhudu juu ya nyumba ya Yakobo, asema Bwana, MUNGU wa majeshi. Kwani katika siku ile nitakapompatiliza Israeli makosa yake, nitazipatiliza pia madhabahu za Betheli, na pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali, na kuanguka chini. Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa joto; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema BWANA.
Amosi 3:9-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Tangazeni katika ikulu za Ashdodi, na katika ikulu za nchi ya Misri: “Kusanyikeni kwenye milima inayoizunguka nchi ya Samaria, mkajionee msukosuko mkubwa na dhuluma zinazofanyika humo.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu hawa wameyajaza majumba yao vitu vya wizi na unyang'anyi. Hawajui kabisa kutenda yaliyo sawa! Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao, atapaharibu mahali pao pa kujihami, na kuziteka nyara ikulu zao.” Mwenyezi-Mungu, asema hivi: “Kama vile mchungaji ampokonyavyo simba kinywani miguu miwili tu au kipande cha sikio la kondoo, ndivyo watakavyonusurika watu wachache tu wa Israeli wakaao Samaria, ambao sasa wanalalia vitanda vizuri na matandiko ya hariri.” Bwana Mungu wa majeshi asema hivi: “Sikilizeni, mkawaonye wazawa wa Yakobo: Siku nitakapowaadhibu Waisraeli kwa sababu ya makosa yao, nitayaharibu pia madhabahu ya mji wa Betheli. Nitazikata pembe za kila madhabahu na kuziangusha chini. Nitaziharibu nyumba zote mjini na vijijini; nitazibomoa nyumba zilizopambwa kwa pembe, majumba makubwamakubwa hayatasalia hata moja. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Amosi 3:9-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tangazeni katika ngome za Ashdodi na katika ngome za Misri: “Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria; angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake, na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.” BWANA asema: “Hawajui kutenda lililo jema, wale ambao hujilundikia nyara na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.” Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi: “Adui ataizingira nchi; ataangusha chini ngome zenu na kuteka nyara maboma yenu.” Hili ndilo asemalo BWANA: “Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba vipande viwili tu vya mfupa wa mguu au kipande cha sikio, hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa, wale wakaao Samaria kwenye kingo za vitanda vyao, na katika Dameski kwenye viti vyao vya fahari.” “Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote. “Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake, nitaharibu madhabahu za Betheli; pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali na kuanguka chini. Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika, pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi; nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,” asema BWANA.

Amosi 3:9-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake. Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang’anyi katika majumba yao. Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara. Haya ndiyo asemayo BWANA; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya semadari, na juu ya mito ya hariri ya kitanda. Sikieni, mkashuhudu juu ya nyumba ya Yakobo, asema Bwana, MUNGU wa majeshi. Kwani katika siku ile nitakapompatiliza Israeli makosa yake, nitazipatiliza pia madhabahu za Betheli, na pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali, na kuanguka chini. Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa hari; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema BWANA.