2 Wafalme 22:19
2 Wafalme 22:19 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa kuwa umetubu na kunyenyekea mbele yangu, hata umerarua mavazi yako na kulia mbele yangu, hapo uliposikia niliyosema dhidi ya mahali hapa na dhidi ya wakazi wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nami pia nimekusikia.
2 Wafalme 22:19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekeza mbele za BWANA, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema BWANA.
2 Wafalme 22:19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekesha mbele za BWANA, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema BWANA.
2 Wafalme 22:19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za BWANA uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake, kwamba wangelaaniwa na kuachwa ukiwa, basi kwa sababu uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema BWANA.