Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Fal 22

22
Yosia Atawala Yuda
1 # 1 Fal 13:2; 1 Nya 3:14; 2 Nya 34:1; Yer 1:2; Sef 1:1; Mt 1:10; Yos 15:39 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi. 2#Kum 5:32; Yos 1:7; Mit 4:27; Eze 18:14-17Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.
Hilkia Agundua Kitabu cha Sheria
3 # 2 Nya 34:8 Ikawa, katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia, mfalme akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, mwandishi, nyumbani kwa Bwana, akisema, 4#2 Fal 12:4,9; 2 Nya 24:8-14; Mk 12:41,42; Neh 11:19; Zab 84:10Enenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, ili aihesabu fedha yote inayoletwa nyumbani mwa BWANA, ambayo mabawabu wameipokea kwa watu; 5#2 Fal 12:11-14tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya BWANA, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba; 6wapewe maseremala, na wajenzi, na waashi; ili kununua miti na mawe yaliyochongwa wapate kuitengeneza nyumba. 7#2 Fal 12:15; Neh 7:2; 1 Kor 4:2Lakini hawakuulizwa habari za ile fedha waliyokabidhiwa; maana walitenda kazi kwa uaminifu.
8 # Kum 31:24; 2 Nya 34:14 Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma. 9Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA. 10#Yer 36:21Kisha Shafani mwandishi akamwambia mfalme, akasema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akakisoma mbele ya mfalme. 11#2 Nya 34:20Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake. 12Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Akbori, mwana wa Mikaya, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme akasema, 13#Zab 25:14; Mit 3:6; Kum 29:27Enendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya BWANA ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa.
14 # Kut 15:20; Amu 4:4; Lk 2:36; 1 Kor 11:5; 2 Nya 34:22 Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye. 15Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu yule aliyewatuma ninyi kwangu, 16#Kum 29:27; Dan 9:11-14BWANA asema hivi, Tazama, mimi nitaleta uovu juu ya mahali hapa, na juu yao wakaao hapa, naam, maneno yote ya kitabu alichokisoma mfalme wa Yuda; 17#Zab 115:4; Isa 2:8,9; 44:17-20; 46:5-8; Mik 5:13kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike. 18#2 Nya 34:26; Mhu 8:12Lakini yule mfalme wa Yuda, aliyewatuma ninyi kumwuliza BWANA, mtamwambia hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa habari ya maneno yale uliyoyasikia, 19#Zab 51:17; Isa 57:15; 66:2; Kut 10:3; Law 26:26-41; 1 Fal 21:29; 2 Nya 33:12; Zab 34:18; 51:17; Lk 14:11; 1 Pet 5:5,6; Yak 4:6,7; Yer 26:6; 44:22kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekesha mbele za BWANA, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema BWANA. 20#Zab 37:37; Isa 57:1,2Kwa hiyo tazama, nitakukusanya pamoja na baba zako, nawe utawekwa kaburini mwako kwa amani; wala macho yako hayatauona uovu huo wote nitakaouleta juu ya mahali hapa. Basi wakamletea mfalme habari tena.

Iliyochaguliwa sasa

2 Fal 22: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia