2 Wakorintho 10:3-6
2 Wakorintho 10:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.
2 Wakorintho 10:3-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika.
2 Wakorintho 10:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia. Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu; tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo. Mkisha kuwa wakamilifu katika kutii, sisi tuko tayari kuadhibu kila namna ya kutotii.
2 Wakorintho 10:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)