2 Mambo ya Nyakati 7:15-16
2 Mambo ya Nyakati 7:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
2 Mambo ya Nyakati 7:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa nitalichunga hekalu hili na kusikiliza maombi yatakayofanyika hapa, kwa maana nimeitakasa nyumba hii ili watu waliabudu jina langu hapa milele. Nitailinda na kuipenda daima.
2 Mambo ya Nyakati 7:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
2 Mambo ya Nyakati 7:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa. Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.