2 Mambo ya Nyakati 20:12-13
2 Mambo ya Nyakati 20:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe ndiwe Mungu wetu! Waadhibu, kwani sisi hatuna uwezo wowote mbele ya jeshi kubwa kama hili linalotujia. Hatujui la kufanya ila tunatazamia msaada kutoka kwako.” Wanaume wote wa Yuda, pamoja na wake zao na watoto wao, walikuwa wamesimama hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 20:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako. Wakasimama Yuda wote mbele za BWANA, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.
2 Mambo ya Nyakati 20:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.” Watu wote wa Yuda pamoja na wake zao, watoto wao na wadogo wao wakasimama pale mbele za BWANA.
2 Mambo ya Nyakati 20:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako. Wakasimama Yuda wote mbele za BWANA, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.