1 Samueli 8:19-21
1 Samueli 8:19-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata hivyo watu walikataa kumsikiliza Samueli, wakasema, “La! Sisi tutakuwa na mfalme juu yetu, ili nasi pia tuwe kama mataifa mengine. Mfalme wetu, atatuhukumu, atatuongoza na kutupigania vita vyetu.” Samueli alipokwisha sikiliza kila kitu walichosema, akaenda na kumweleza Mwenyezi-Mungu.
1 Samueli 8:19-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atuongoze na kupigana vita vyetu Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA.
1 Samueli 8:19-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA.
1 Samueli 8:19-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.” Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za BWANA.