1 Samueli 2:1-2
1 Samueli 2:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
1 Samueli 2:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
1 Samueli 2:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Halafu Hana aliomba na kusema: “Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu. Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu. Nawacheka adui zangu; maana naufurahia ushindi wangu. “Hakuna aliye mtakatifu kama Mwenyezi-Mungu; hakuna yeyote aliye kama yeye; hakuna aliye mwamba kama Mungu wetu.
1 Samueli 2:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Hana akaomba na kusema: “Moyo wangu wamshangilia BWANA, katika BWANA pembe yangu imeinuliwa juu. Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako. “Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama BWANA, hakuna mwingine zaidi yako; hakuna Mwamba kama Mungu wetu.