1 Samueli 10:15-16
1 Samueli 10:15-16 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” Sauli akajibu, “Alituhakikishia kwamba punda wamepatikana.” Lakini hakumwambia babaye mdogo kila kitu Samweli alichomwambia kuhusu ufalme.
1 Samueli 10:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Shauli akajibu, “Alituambia waziwazi kuwa punda wamepatikana.” Lakini Shauli hakumweleza kuwa Samueli alimwambia kuwa atakuwa mfalme.
1 Samueli 10:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali niambie, huyo Samweli aliwaambiaje? Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja.
1 Samueli 10:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali uniambie, huyo Samweli aliwaambiaje? Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja habari hiyo.