1 Wafalme 17:21-24
1 Wafalme 17:21-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena. BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai. Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la BWANA kinywani mwako ni kweli.
1 Wafalme 17:21-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumlilia BWANA, akisema, “Ee BWANA Mungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!” BWANA akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!” Ndipo yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la BWANA kutoka kinywani mwako ni kweli.”
1 Wafalme 17:21-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Elia akajinyosha juu ya mtoto huyo mara tatu na kumwomba Mwenyezi-Mungu, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, mrudishie mtoto huyu roho yake!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi la Elia; mtoto akaanza kupumua tena. Elia akamrudisha mtoto chini kwa mama yake, akamwambia, “Tazama! Mwanao yu hai.” Huyo mwanamke mjane akamwambia Elia, “Sasa najua kwa hakika kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na maneno aliyokupa Mwenyezi-Mungu uyaseme ni ya kweli.”
1 Wafalme 17:21-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena. BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka ghorofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai. Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la BWANA kinywani mwako ni kweli.