Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 17

17
Eliya atabiri ukame
1 # Lk 1:17; 4:25; 2 Fal 3:14; Kum 10:8; Yak 5:17 Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu. 2Neno la BWANA likamjia, kusema, 3Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. 4#Zab 37:3; Isa 33:15 Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 5Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa alikwenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. 6Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. 7Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
Mjane wa Sarepta
8Neno la BWANA likamjia, kusema, 9#Oba 1:20; Lk 4:26 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.
10 # Mwa 24:7; Zab 24:1; Isa 33:16; Yn 4:7; Ebr 11:37 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12#Mwa 18:6; 21:15,16 Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule kisha tufe. 13#Mwa 22:1,2; 1 Pet 1:7 Eliya akamwambia, Usiogope; nenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujitengenezee na mwanao. 14#Zab 84:7-10,12; 34:11; 1 Tim 4:8; Flp 4:19 Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi. 15#2 Nya 20:20; Mt 10:41,42; 20:28; Ebr 11:8 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16#Kum 15:10; Mit 11:24 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
Eliya amfufua mtoto wa mama mjane
17Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena. 18#2 Sam 16:10; Lk 4:34; 5:8; Yn 2:4 Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu? 19Akamwambia, Nipe mwanao. Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake. 20#Kut 15:25; 17:4; Hes 11:11; 1 Sam 7:8; 1 Fal 18:36,37; Flp 4:6; Yak 5:13,16 Akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumwua mwanawe? 21#2 Fal 4:34,35; Mdo 20:10 Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena. 22#Zab 65:2; 66:19; Mit 15:8,29; Mt 21:22; Lk 11:9,10; 1 Yoh 3:22; 5:14; Kum 32:39; Lk 7:14; Mdo 20:10,12; Ebr 11:35 BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. 23Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka ghorofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai. 24#Yn 3:2; 16:30 Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la BWANA kinywani mwako ni kweli.

Iliyochaguliwa sasa

1 Wafalme 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha