1 Wafalme 17:2-7
1 Wafalme 17:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Elia: “Ondoka hapa uelekee mashariki, ukajifiche penye kijito cha Kerithi kilichoko mashariki ya mto Yordani. Huko, utapata maji ya kunywa katika kijito hicho tena nimewaamuru kunguru wakuletee chakula.” Basi, Elia akatii agizo la Mwenyezi-Mungu, akaenda kukaa kwenye kijito cha Kerithi kilichoko mashariki ya mto Yordani. Kunguru wakawa wanamletea mkate na nyama, asubuhi na jioni; akapata na maji ya kunywa katika kijito hicho. Lakini, baada ya siku chache kijito kikakauka kwa sababu hapakunyesha mvua nchini.
1 Wafalme 17:2-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa alikwenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
1 Wafalme 17:2-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
1 Wafalme 17:2-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha neno la BWANA likamjia Eliya, kusema, “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. Utakunywa maji kutoka kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.” Hivyo akafanya kile alichoambiwa na BWANA. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki ya Yordani na akakaa huko. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito. Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi.