1 Yohane 3:4-6
1 Yohane 3:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria. Mnajua kwamba Kristo alikuja kuziondoa dhambi zetu, na kwamba kwake hamna dhambi yoyote. Basi, kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi dhambi; lakini kila mtu atendaye dhambi hakupata kamwe kumwona wala kumjua Kristo.
1 Yohane 3:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
1 Yohane 3:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi. Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi. Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua.
1 Yohane 3:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)