1 Wakorintho 4:14-21
1 Wakorintho 4:14-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha nyinyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi. Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema. Kwa hiyo, nawasihi: Fuateni mfano wangu. Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote. Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu. Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya. Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu. Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?
1 Wakorintho 4:14-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi, nawasihi mnifuate mimi. Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa. Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu. Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu wajivunao, bali nguvu zao. Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?
1 Wakorintho 4:14-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi, nawasihi mnifuate mimi. Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa. Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu. Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao. Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?
1 Wakorintho 4:14-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Siwaandikii mambo haya ili kuwaaibisha, bali ili kuwaonya, kama wanangu wapendwa. Hata kama mnao walimu 10,000 katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili. Basi nawasihi igeni mfano wangu. Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Kristo Yesu, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa. Baadhi yenu mmekuwa na jeuri mkidhani kuwa sitafika kwenu. Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao. Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?