1 Wakorintho 16:13-24
1 Wakorintho 16:13-24 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari. Fanyeni kila kitu katika upendo. Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio walikuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi, mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii. Nilifurahi Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa. Makundi ya waumini wa jimbo la Asia wanawasalimu. Akila na Prisila pamoja na kundi la waumini walioko nyumbani mwao wanawasalimu sana katika Bwana Isa. Ndugu wote walio hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kama mtu yeyote hampendi Bwana Isa Al-Masihi, na alaaniwe. Bwana wetu Isa, njoo. Neema ya Bwana Isa iwe nanyi. Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Al-Masihi Isa. Amen.
1 Wakorintho 16:13-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu. Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo. Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi nyinyi ndugu zangu, muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumika pamoja nao. Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu. Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii. Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priska pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika kuungana na Bwana. Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu. Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe. Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANATHA – BWANA, NJOO! Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. Upendo wangu uwe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu.
1 Wakorintho 16:13-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kesheni, simameni imara katika imani, iweni na ujasiri, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumia watakatifu); watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao. Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha. Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.
1 Wakorintho 16:13-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu); watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao. Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha. Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.