1 Mambo ya Nyakati 4:10
1 Mambo ya Nyakati 4:10 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Yabesi alimwomba Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, nakusihi unibariki na kuipanua mipaka yangu. Mkono wako uwe pamoja nami na unilinde kutokana na jambo lolote ovu, lisiniumize.” Naye Mungu akamjalia yale aliyoomba.
1 Mambo ya Nyakati 4:10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
1 Mambo ya Nyakati 4:10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
1 Mambo ya Nyakati 4:10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.