Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ruthu UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki kidogo kimepewa jina la mtu mashuhuri katika simulizi hili, yaani Ruthu. Umaarufu wa Ruthu unaweza kutazamwa kwa namna mbili. Kwanza kabisa Ruthu ni mwanamke (kitabu kingine katika Biblia kinachojulikana kwa jina la mwanamke ni kile tu cha Esta na kile cha Yudithi, hiki cha pili, yaani Yudithi, kikiwa katika orodha ya vitabu vya kutoka Deuterokanoni). Pili, tofauti na Esta ambaye alikuwa Mwisraeli, Ruthu hakuwa Mwisraeli. Labda tamko lake kwa mama mkwe wake: “Mungu wako atakuwa Mungu wangu” (1:6b) linadhihirisha pia ushujaa wake huyu ambaye ataorodheshwa kama mmoja wa ukoo wa Daudi.
Kitabu chenyewe kinafuata kitabu cha Waamuzi kulingana na Septuajinta, labda kwa sababu ya habari inayotajwa hapo mwanzoni ambayo inagusia nyakati za Waamuzi yaani: “Wakati waamuzi walipokuwa wanatawala Israeli”. Lakini katika Biblia ya Kiebrania kimewekwa kati ya kitabu cha Methali na kile cha Wimbo Bora.
Hadithi ya Ruthu yahusu mambo au hali ilivyokuwa huko Kanaani kabla ya kuanzishwa utawala wa kifalme. Simulizi lenyewe laanza kwa kumtaja mama mmoja Mmoabu, Ruthu, ambaye alikuwa ameolewa katika jamii ya Waisraeli, kisha kwa sababu ya njaa wakahamia katika nchi ya Moabu. Wakiwa huko Mumewe alifariki, kisha yeye na mamamkwe wake walirudi mpaka nchini Israeli ambako alimpata mwanamume wa jamaa ya mumewe marehemu, akamwoa.
Mwishoni mwa kijitabu hiki yamkini maana ya jumla ya hilo simulizi ni dhahiri: Kutayarisha limbuko la mfalme Daudi. Ruthu ni mmoja wa akina mama katika nasaba ya Daudi.
Licha ya shabaha hiyo ya kitabu hiki, jambo moja pia ni dhahiri: Baraka kuu za Mungu hupewa pia watu wasio wa jumuiya ya Israeli. Ndio kusema Mwenyezi-Mungu siyo tu Mungu wa watu wa Israeli bali pia wa watu wasio Waisraeli.

Iliyochaguliwa sasa

Ruthu UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia