Zaburi 60:6-12
Zaburi 60:6-12 BHN
Mungu amesema kutoka patakatifu pake “Sasa nitaigawa Shekemu kwa shangwe, Bonde la Sukothi nitalipima sehemusehemu. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya enzi. Moabu ni kama bakuli langu la kunawia, kiatu changu nitaitupia Edomu kuimiliki. Nitapiga kelele ya ushindi juu ya Filistia.” Ni nani atakayenipeleka kwenye mji wa ngome? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu? Je, umetuacha kabisa, ee Mungu? Wewe huendi tena na majeshi yetu! Utupatie msaada dhidi ya maadui zetu, maana msaada wa binadamu haufai kitu. Mungu akiwa upande wetu tutashinda, yeye atawaponda maadui zetu.