Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 56

56
Kumtumainia Mungu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo “Njiwa Mkimya wa Mbali”. Utenzi wa Daudi baada ya kukamatwa na Wafilisti kule Gathi)
1Ee Mungu, unionee huruma,
maana watu wananishambulia.
Mchana kutwa maadui wananidhulumu.
2Mchana kutwa maadui zangu wananishambulia;
ni wengi mno hao wanaonipiga vita.
3Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika,
mimi nakutumainia wewe.
4Namtumainia Mungu na kusifu neno lake;
namtumainia Mungu, wala siogopi.
Binadamu dhaifu atanifanya nini?
5Mchana kutwa wanapotosha kisa changu;
mawazo yao yote ni ya kunidhuru.
6Wanakutana kupanga na kunivizia;
wanachunguza yote nifanyayo;
wananiotea kwa shabaha ya kuniua.
7Ee Mungu, uwalipe kwa kadiri ya uovu wao,
uwaangushe hao waovu kwa hasira yako.
8Wewe wakujua kusukwasukwa kwangu;
waweka kumbukumbu ya machozi yangu yote.
Je, yote si yamo kitabuni mwako?
9Kila mara ninapokuomba msaada wako,
maadui zangu wanarudishwa nyuma.
Najua kweli Mungu yuko upande wangu.
10Namtumaini Mungu na kusifu neno lake;
namtumainia Mwenyezi-Mungu na kusifu neno lake.
11Namtumainia Mungu, wala siogopi.
Binadamu atanifanya nini?
12Ee Mungu, nitatimiza ahadi zangu kwako;
nitakutolea tambiko za shukrani,
13Maana umeniokoa katika kifo,
naam, umenilinda nisianguke chini;
nipate kuishi mbele yako, ee Mungu,
katika mwanga wa uhai.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 56: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha