Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 3:1-8

Zaburi 3:1-8 BHN

Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu, ni wengi mno hao wanaonishambulia. Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Sitayaogopa maelfu ya watu, wanaonizingira kila upande. Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru. Mwenyezi-Mungu ndiwe uokoaye; uwape baraka watu wako.

Soma Zaburi 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 3:1-8

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha