Zaburi 22:1-3
Zaburi 22:1-3 BHN
Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Mbona uko mbali sana kunisaidia, mbali na maneno ya kilio changu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu; napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati. Hata hivyo, wewe ni mtakatifu; wewe watawala na kusifiwa na Waisraeli.