Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 137:1-9

Zaburi 137:1-9 BHN

Kando ya mito ya Babuloni, tulikaa, tukawa tunalia tulipokumbuka Siyoni. Katika miti ya nchi ile, tulitundika zeze zetu. Waliotuteka walitutaka tuwaimbie; watesi wetu walitutaka tuwafurahishe: “Tuimbieni mojawapo ya nyimbo za Siyoni!” Twawezaje kuimba wimbo wa Mwenyezi-Mungu katika nchi ya kigeni? Ee Yerusalemu, kama nikikusahau, mkono wangu wa kulia na ukauke! Ulimi wangu na uwe mzito, kama nisipokukumbuka wewe, ee Yerusalemu; naam, nisipokuthamini kuliko furaha yangu kubwa! Ee Mwenyezi-Mungu, usisahau waliyotenda Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipotekwa; kumbuka waliyosema: “Bomoeni mji wa Yerusalemu! Ngoeni hata na misingi yake!” Ee Babuloni, utaangamizwa! Heri yule atakayekulipiza mabaya uliyotutenda! Heri yule atakayewatwaa watoto wako na kuwapondaponda mwambani!

Soma Zaburi 137

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 137:1-9