Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 121

121
Mungu kinga yetu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1Natazama juu milimani;
msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.
3Hatakuacha uanguke;
mlinzi wako hasinzii.
4Kweli mlinzi wa Israeli
hasinzii wala halali.
5Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;
yuko upande wako wa kulia kukukinga.
6Mchana jua halitakuumiza,
wala mwezi wakati wa usiku.
7Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote;
atayalinda salama maisha yako.
8Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote#121:8 … katika shughuli zako zote: Kiebrania: Uingiapo na utokapo, kwa maana ya jumla, popote uendapo au ulipo.
tangu sasa na hata milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 121: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia