Zaburi 110
110
Kutawazwa kwa mfalme mteule
(Zaburi ya Daudi)
1 # Taz Mat 22:44; Marko 12:36; Luka 20:42:43; Mate 2:34-35; 1Kor 15:25; Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu:
“Keti upande wangu wa kulia,
hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
2Mwenyezi-Mungu ataeneza enzi yako kutoka Siyoni;
utatawala juu ya maadui zako wote.
3Watu wako watakujia kwa hiari,
siku utakapokwenda kuwapiga maadui.
Juu ya milima mitakatifu watakujia vijana wako,
kama umande unaotokeza alfajiri mapema.#110:3 Kigiriki (Septuaginta) Kwako ni cheo cha kifalme tangu ulipozaliwa juu ya milima mitakatifu. Kutoka tumboni, kabla ya pambazuko, nilikuzaa.
4 # Taz Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21 Mwenyezi-Mungu amekuapia wala hatabadili nia yake:
“Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”
5Bwana yuko upande wako wa kulia;
atawaponda wafalme atakapokasirika.
6Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi;
atawaponda viongozi kila mahali duniani.
7Mfalme atakunywa maji ya kijito njiani;
naye atainua kichwa juu kwa ushindi.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 110: BHN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.