Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 30:18-23

Methali 30:18-23 BHN

Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, naam, mambo manne nisiyoyaelewa: Njia ya tai angani, njia ya nyoka mwambani, njia ya meli baharini, na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke. Mwenendo wa mwanamke mwasherati ni hivi: Yeye hula, akajipangusa mdomo, na kusema, “Sijafanya kosa lolote!” Kuna mambo matatu ambayo huitetemesha dunia, naam, mambo manne ambayo haiwezi kuyastahimili: Mtumwa anayekuwa mfalme; mpumbavu anayeshiba chakula; mwanamke asiyependwa anayeolewa; na mjakazi achukuapo nafasi ya bibi yake.

Soma Methali 30