Mithali 30:18-23
Mithali 30:18-23 NEN
“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyovielewa: Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. “Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi, hula akapangusa kinywa chake na kusema, ‘Sikufanya chochote kibaya.’ “Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia: Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula, mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.