Methali 3:21-24
Methali 3:21-24 BHN
Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, navyo vitakuwa uhai nafsini mwako, na pambo zuri shingoni mwako. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama, wala mguu wako hautajikwaa. Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu.