Methali 29:22-27
Methali 29:22-27 BHN
Mwenye ghadhabu huchochea ugomvi, mtu wa hasira husababisha makosa mengi. Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima. Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe; husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno. Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe, lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama. Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu. Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.